Gazeti la The Jakarta Post limeripoti kuwa mashindano hayo ni sehemu ya mashindano ya taifa ya Qur'ani ambayo hufanyika kila mwaka kote nchini Indonesia kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi.
Karibu wanafunzi 252 wa shule za msingi wanashiriki katika mashindano hayo ambayo pia yanajumuisha usomaji mashairi, kaligrafia ya Kiislamu na maarifa ya dini.
Lengo la mashindano hayo limetajwa kuwa ni kuzidisha maarifa ya wanafunzi wa shule za msingi na juhudi za kuifanya Indonesia kuwa taifa la Kiislamu.
Indonesia ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya jamii ya Waislamu duniani. Nchi hiyo ina jamii ya watu milioni 242 na asilimia 90 kati yao ni Waislamu, asilimia 8 Wakristo na asilimia 2 ni Wahindu na Mabudha.
Nchi hiyo ina misikiti laki tano na khamsini elfu. 784207