Kituo cha habari cha Nowlebanon kimeripoti kuwa taarifa ya Hizbullah imesema kutiwa saini mapatano ya kitaifa ya Palestina ni ishara ya kuungana makundi yaliyodhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
Hizbullah imeongeza kuwa makubaliano hayo ya suluhu yameimarisha mapambano ya ukombozi wa Palestina na kuzidisha nguvu ya harakati za mapambano dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
Taarifa hiyo imeashiria jinsi Marekani na Israel zilivyochukizwa na mapatano hayo na kusema suala hilo ni hatua sahihi ambayo itanufaisha mapambano ya ukombozi ya tafa la Palestina.
Hizbullah imesema makubaliano ya Hamas na Fat'h ni matunda ya kwanza ya mapinduzi ya wananchi wa Misri na inatazamiwa kuwa ilitarejesha hadhi na heshima ya nchi hiyo katika suala la kutetea masuala ya ulimwengu wa Kiislamu.
Hamas na Fat'h zimetia saini makubaliano ya mapatano ambayo yanatayarisha njia ya kuitishwa chaguzi za rais na bunge. 783667