Wizara ya Ulinzi ya Iran imesema mashindano hayo yatajumuisha vitengo vya qiraa, tarteel, ufahamu na tafsiri.
Taarifa ya Wizara ya Ulinzi imesema mashindano hayo yatakuwa ya kiwango cha juu na jopo la majaji litajumuisha majaji wenye uzoefu wa kimataifa.
Mashindano hayo yatakuwa na washiriki 135 wa kike wanaofanya kazi katika Jeshi la Iran, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Jeshi la Polisi, Wizara ya Ulinzi na Makao Makuu ya Vikosi Vyote vya Kijeshi vya Iran.
767867