Kwa mujibu wa tovuti ya atlasinfo maandamano hayo ambayo yanafanyika chini ya anwani ya 'Akina mama wavaa-hijabu' yanalalamikia hatua ya walimu wa shule za mji huo ya kuwakosea heshima akina mama na mabinti wa Kiislamu wanaovaa hijabu mjini humo.
Maandamano hayo yamepangwa kufanyika leo kuanzia saa kumi kwa wakati wa Ufaransa kuanzia uwanja mkuu wa mji wa Montreuil kuelekea makao makuu ya Idara ya Usimamizi na Masomo ya Kitaifa ambapo waandamanaji watataka malalamiko yao yashughulikiwe mara moja.
Baadhi ya shule za mji huo zimepiga marufuku akina mama wanaovaa hijabu kuandamana na watoto wao katika ratiba maalumu za masomo.
Sheria za Ufaransa zinawazuia wanafunzi tu kushiriki masomo wakiwa wamevaa hijabu na wala sio wazazi wao wanaoandamana nao kwenye masomo hayo. 784303