Taarifa ya muungano huo imeashiria hali ya Libya na kulaani mauaji yanayofanywa na askari wa Muammar Gaddafi na vibaraka wake dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia yoyote.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeashiria hali ya Yemen na kuyataka makundi yote ya nchi hiyo kufanya juhudi za kuliunganisha taifa hilo na vyama vyote vya kisiasa na kujiepusha na hitilafu na migawanyiko.
Mapinduzi ya wananchi wa Misri na Tunisia pia yameashiriwa katika taarifa ya Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu. Taarifa hiyo imesisitiza juu ya kuimarishwa uwekezaji katika sekta ya utalii kwa shabaha ya kuboresha uchumi wa nchi hizo.
Vilevile imezungumzia mapatano yaliyofikiwa kati ya makundi ya Hamas na Fat'h huko Palestina na hali ya ndani ya Somalia.
Hata hivyo taarifa ya Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu imepuuza kabisa mauaji yanaoendelea kufanywa dhdi ya wananchi wa Bahrain. Muungano huo unadhibitiwa na taasisi za Saudi Arabia. 785229