IQNA

OIC yasema ugaidi hautaangamia kwa kuuawa bin Laden

13:42 - May 03, 2011
Habari ID: 2116552
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC amesema kuwa, mizizi ya ugaidi haiwezi kung'olewa kwa kuuawa kiongozi wa mtangao wa al-Qaeda Usama bin Laden.
Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu amesema katika radiamali yake kuhusiana na habari ya kuuawa Usama bin Laden kwamba, Bin Laden na wanachama wa kundi lake la kigaidi la al-Qaeda wamewauwa watu wengi wasio na hatia katika maeneo mbalimbali ulimwenguni. Katibu Mkuu wa OIC amesema bayana kwamba, Jumuiya ya Nchi za Kiislamu inalaani kwa nguvu zake zote vitendo vyovyote vile vya kigaidi na kwamba, kufanya mauaji sio njia mwafaka ya kung'oa mizizi ya ugaidi bali kuna haja ya kutafuta chanzo na kisha kupambana na chanzo hicho cha ugaidi.
Kadhalika Katibu Mkuu wa OIC ameashiria kuongezeka harakati za wananchi za kupigania haki na uadilifu katika Mashariki ya Kati na kusisitiza kwamba, wananchi wa mataifa ya Mashariki ya Kati wanataka kuwa na maisha bora.
785632
captcha