IQNA

Kituo cha dini kuanzishwa Uswisi

13:01 - May 04, 2011
Habari ID: 2117263
Bunge la mji mkuu wa Uswisi, Bern, limepitisha muswada wa kujengwa kituo cha kidini mjini humo kufikia mwanzoni mwa mwaka 2014.
Kwa mujibu wa tovuti ya Saphirnews kituo hicho kitaanzishwa kwa madhumuni ya kuimarisha mazungumzo ya kidini kati ya dini za Uislamu, Ukristo, Uyahudi, Uhindu na Ubudha. Kituo hicho kitajengwa kwa msaada wa serikali na wafuasi wa dini hizo. Gharama ya ujenzi wake inakadiriwa kufikia euro 150,000. Mswada huo ulikuwa umepangwa kupitishwa mwaka uliopita lakini uliakhirishwa kutokana na mvutano uliozuka nchini humo kati ya wafuasi wa dini mbalimbali na wabunge wenye misimamo ya kupindukia mipaka wanaopinga kujengwa vituo vya kidini nchini Uswisi, kufuatia kupigwa marufuku ujenzi wa minara kwenye misikiti ya nchi hiyo. 786448
captcha