Kituo cha habari cha al-Islam kimeripoti kuwa mjumuiko huo utakaohudhuriwa na watu waliongia katika Uislamu nchini Uswisi utafanyika Lausanne kwa mara ya kwanza kabisa kwa hima ya Msikiti na Kituo cha Kiislamu cha mji huo.
Lengo la kuainisha Siku ya Kitaifa ya Waislamu Wapya nchini Uswsi ni kuwakutanisha pamoja ili watambuane na kutayarisha mazungumzo kuhusu sababu zinazowafanya watu wa dini mbalimbali wakubali dini ya Kiislamu.
Uislamu ni dni ya pili kwa kuwa na wafuasi wengi nchini Uswisi na inakadiriwa kuwa asilimia nne ya watu wa nchi hiyo ni Waislamu.
Hata hivyo mwaka uliopita wa 2010 serikali ya Uswisi ilipiga marufuku ujenzi wa minara ya misikiti nchini humo suala ambalo lilipingwa vikali na jumuiya za kutetea haki za kiraia na uhuru wa kuabudu, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na mashirika ya kutetea haki za binadamu. 786469