Sherehe hiyo itafanyika Mei 5 katika Chuo Kikuu cha Sayansi za Kiislamu katika mji mtakatifu wa Mash'had.
Idara ya Uhusiano wa Kiislamu katika taasisi ya Astan-e-Quds Razavi imesema waalimu watakaoenziwa wanafundisha tafsiri ya Qur'ani, hadithi, hifdhi na qiraa. Waalimu hao wanafundisha katika Chuo cha Mahd-u-Reza ambacho kinafungamana na Kitivo cha Qur'ani na Hadithi katika Chuo Kikuu cha Sayansi za Kiislamu.
Taasisi ya Astan-e-Quds Razavi inasimamia Haram Takatifu ya Imam Ridha AS katika mji wa Mash'had. Taasisi hiyo mbali na kusimamia haram hiyo takatifu pia inajishughulisha na harakati kadhaa za Kiislamu na kiutamaduni.
786738