IQNA

Mafunzo ya majaji wa mashindano ya Qur'ani kuanza mjini Riyadh

12:36 - May 05, 2011
Habari ID: 2117739
Duru ya tano ya mafunzo ya majaji wa mashindano ya Qur'ani itaanza tarehe 7 Mei katika hoteli ya Qasr kwenye mji mkuu wa Saudi Arabia Riyadh chini ya usimamizi wa Wizara ya Wakfu na Masala ya Kiislamu.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mashindano ya 13 ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani ya Saudia na yatawashirikisha wanafunzi 31 wa kike na kiume.
Lengo la mafunzo hayo limetajwa kuwa ni kutayarisha majaji na kukuza uwezo wao wa kielimu kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya ndani na ya kimataifa ya Qur'ani.
Majaji wanaoshiriki katika mafunzo hayo wanachaguliwa na Jumuiya ya Masuala ya Kheri na Kuhifadhisha Qur'ani na kupasishwa na sekretarieti ya mashindano ya kitaifa ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu ya Saudi Arabia. 786507

captcha