IQNA

Kongamano la harakati za Qur’ani Tehran

14:08 - May 08, 2011
Habari ID: 2118597
Msikiti wa Imam Sadeq AS Mei tisa utakuwa mwenyeji wa kongamano la wanaharakati na maqari wa Qur'ani mjini Tehran.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kongamano hilo kufanyika katika mwaka huu wa Kiirani-Hijria Shamsia-ulioanza Machi 21.
Kongamano hilo limeandaliwa na ‘Nyumba ya Qur’ani ya Utamaduni’ na lengo limetajwa ni kuwaenzi wanaharakati waandamizi wa Qur’ani mjini Tehran na kujadili njia za kubuni jumuiya ya wanaharakati wa Qur’ani.
Kongamano la harakati za Qur’ani Tehran lilifanyika kwa mara ya kwanza mwezi Novemba mwaka 2009 na kuhudhuriwa na maqari wa kimataifa na wasomi wengine wa Qur’ani.
Msikiti wa Imam Sadeq AS ulio katika Medani ya Palestina umekuwa mwenyeji wa mikutano kadhaa ya Qur’ani.
767875
captcha