IQNA

Madrasa ya Qur'ani ya Dar al-Fidous yafunguliwa Senegal

15:57 - May 08, 2011
Habari ID: 2118697
Madrasa ya Qur'ani kwa jina la Dar al-Firdaous ilifunguliwa jana Jumamosi huko katika mji wa Thies nchini Senegal.
Lugha za Kiarabu na Kifaransa zitatumika katika kuwafundisha wanafunzi wataoshiriki masomo ya Qur'ani katika shule hiyo.
Akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa shule hiyo, Bubakr Andow, mkuu wa shule hiyo ameashiria umuhimu wa mafunzo ya Qur'ani na kuongeza kuwa kila Muislamu anayetaka kujifunza misingi ya dini yake anapasa kuweka mafundisho ya Qur'ani katika ratiba ya shughuli zake za kila siku maishani.
Amewataka maimamu wa swala za jamaa na walimu wa masomo ya dini kuongeza maradufu juhudi zao za kufundisha masomo hayo kwa wanafunzi ili kwa njia hiyo waweze kuchangia juhudi za kupambana na matatizo ya kijamii na kimaanawi nchini.
Kutoa masomo ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu, misingi ya dini na lugha za Kiarabu na Kifaransa ni miongoni mwa ratiba muhimu za masomo ya shule hiyo ya Qur'ani. 787793
captcha