IQNA

Kikao cha kimataifa cha 'Uchumi wa Kiislamu' chaanza nchini Tunisia

16:01 - May 08, 2011
Habari ID: 2118699
Kikao cha kwanza cha Uchumi wa Kiislamu kilianza jana Jumamosi huko Tunis, mji mkuu wa Tunisia.
Kikao hicho cha siku mbili ambacho kinawashirikisha wanauchumi na wataalamu wa masuala ya kiuchumi na kifedha kutoka pembe mbalimbali za dunia, kimeandaliwa na Jumuiya ya Uchumi wa Kiislamu ya Tunisia kwa ushirikiano wa Benki ya Kiislamu ya Zeituna. Akizungumza katika kikao cha siku ya kwanza, Izzu Deen Khoja, Katibu Mkuu wa Baraza la Benki na Taasisi za Uchumi wa Kiislamu la Tunisia amesem kwamba amefurahishwa sana na kuongezeka kwa mashirika na taasisi za uchumi wa Kiislamu katika nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu. Katika hali ya hivi sasa kuna karibu mashirika ya kifedha ya Kiislamu yapatayo 540 duniani na kwamba idadi hiyo inaongezeka kwa asilimia 28 kila mwaka. Amesema taratibu mifumo ya kifedha isiyokuwa ya Kiislamu ambayo inatawala katika nchi za Magharibi imekuwa ikitaka kunufaika na mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu kutokana na faida nyingi zinazopatikana humo, na hasa kufuatia mgogoro mkubwa wa kiuchumi wa hivi karibuni katika nchi hizo. Washiriki wa kikao cha Tunisia wametaka kubuniwa na kutekeleza sheria zinazoambatana na uchumi wa Kiislamu nchini humo kwa kutilia maanani kuwa kuna upungufu na uhaba mkubwa unaohisika katika uwanja huo. Bima za Kiislamu na jinsi ya matumizi yake katika nchi zisizo za Kiislamu ni suala muhimu ambalo limejadiliwa katika siku ya pili ya kikao hicho. 787957
captcha