Mwakilishi wa makabila ya Iraq Basim al Hijami amesema makabila hayo yatafungua mashtaka dhidi ya kasisi wa Kimarekani Terry Jones kutokana na kitendo chake kiovu cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu.
Amesema wakuu wa makabila hayo ya Iraq wanafuatilia kwa karibu maudhui ya kufikishwa mahakamani kasisi huyo Mmarekani.
Basim al Hijami ameongeza kuwa watu wote wanaopenda kheri duniani wanapaswa kuelewa kwamba Qur'ani Tukufu na Uislamu ni anwani ya upendo, amani na usalama na kwamba madharau ya kasisi huyo wa Kimarekani yamewachukiza mno Waislamu kote duniani.
Hatua ya kasisi huyo ya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu imelaaniwa na Waislamu kote duniani. 787403