Kwa mujibu wa gazeti la ad-Dastur linalochapishwa nchini humo, chuo hicho mbali na kuchukua wanachuo kutoka nchi za Kiislamu na Kiarabu kitachukua wanafunzi pia kutoka nchi za Asia na Afrika ambao watahitimu masomo yao katika viwango vya shahada ya kwanza, ya pili na uzamivu katika usomaji Qur'ani na masomo mengine ya kitabu hicho kitakatifu.
Wanachuo watakuwa wakifundishwa na wahadhiri mahiri katika nyanja za usomaji Qur'ani na utafiti wa taaluma mbalimbali za Qur'ani za Kiislamu. Wanachuo watakaohitimu masomo yao katika viwango vya shahada tofauti watapewa pia vibali vya kusoma Qur'ani katika pembe mbalimbali za dunia. Wanachuo waliohitimu masomo katika chuo hicho pia watapewa nafasi ya kuhudumu kama maimamu na mahatibu katika sehemu tofauti katika nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu.
Ni muhimu kuashiria hapa kwamba wanachuo wahitimu watalazimika kusoma visomo vyote kumi vinavyotumika katika usomaji Qur'ani. 788421