"Tuna furaha kushirikiana na Kitivo cha Masomo ya Kiislamu cha Qatar katika kuendesha kozi hii muhimu. Hitajio la bidhaa na huduma za kifedha za Kiislamu linaongezeka kwa kasi isiyo na kifani", amesema mwenyekiti wa Benki ya Kwanza ya Uwekezaji ya Qatar Abdullah bin Fahd bin Ghorab al-Marri.
Kitivo cha Masomo ya Kiislamu cha Qatar kina nafasi muhimu katika kusambaza ufahamu kuhusu turathi ya Kiislamu hasa katika miamala ya kifedha. Kitivo hicho pia kinasaidia kubadilishana uzoefu ambao unasaidia kustawi huduma za kifedha za Kiislamu nchini Qatar ili kukabiliana na changamoto za kiuchumu za zama hizi, amesema mku wa kitivo hicho Hatem al Qaranshawi.
Tayari wanafunzi 220 wa kiume na kike wakiwemo wafanyakazi wa sekta ya Kiislamu ya kifedha wanashiriki katika kozi hiyo ambayo imetayarishwa na Ali al Quradahi mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Qatar.
Yaliyomo katika kozi hiyo ni pamoja na 'kuarifisha uchumi wa Kiislamu' na 'mbinu ya fiqhi ya Kiislamu'.
788427