IQNA

Kongamano la Maafa ya Wananchi wa Libya na Taathira Zake

19:35 - May 09, 2011
Habari ID: 2119461
Kongamano la Maafa ya Wananchi wa Libya na Taathira Zake katika Ulimwengu wa Kiislamu limepangwa kufanyika tarehe 14 Mei mjini Dakar nchini Senegal.
Kongamano hilo linasimamiwa na Jumuiya ya Urafiki na Kuwaunga Mkono Wananchi wa Libya nchini Senegal kwa kushirikiana na jumuiya nyingine za Kiislamu.
Wasimamizi wa kongamano hilo la kitaifa pamoja na wanafikra, maulamaa wa Kiislamu, maimamu wa swala za jamaa na wataalamu wa masuala ya kisiasa wa Senegal watahutubia kongamano hilo kuhusu mapambano ya wananchi wa Libya, mauaji yanayofanywa na serikali ya Gaddafi dhidi ya wapinzani na taathira za machafuko Libya katika nchi nyingine za Kiafrika. 788780



captcha