IQNA

Mehmanparast:

Nchi za eneo zisitumbukie katika fitina ya Marekani na Wazayuni

16:54 - May 11, 2011
Habari ID: 2120200
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Ramin Mehmanparast ameziitaka nchi za eneo la Mashariki ya Kati kuchukua tahadhari ili zisitumbukie katika fitina ya Marekani na Wazayuni yenye lengo la kuibua hitilafu baina ya nchi za eneo hilo.
Akizungumza Mei 10 katika mkutano wa kila wiki na waandishi wa habari mjini Tehran ameongeza kuwa kuimarishwa mashirikiano ya pande mbili na kieneo kunadhamini uthabiti na usalama wa Mashariki ya Kati.
Ramin Mehmanparast ameashiria safari za hivi majuzi za Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika nchi za eneo hili na kuongeza kuwa Tehran daima inahimiza mashirikiano ya pande mbili na ya kieneo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameyasema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi mjini Tehran.
Mehmanparast amesema kuhusiana na matukio ya Bahrain na kukandamizwa wananchi wasio na ulinzi wala hatia wa nchi hiyo kwamba, ukandamizaji na utumiaji mabavu wa aina yoyote dhidi ya wananchi hao wanaotaka kutekelezewa matakwa yao kwa njia ya amani, si sahihi.
789314
captcha