IQNA

Hujjatul Islam Mahdi Taeb:

Kupambana na Wazayuni ndio ufunguo wa mafanikio

17:06 - May 11, 2011
Habari ID: 2120205
Kupambana na Utawala wa Kizayuni kunapaswa kuwa moja ya malengo ya mwamko wa wananchi katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kwani uzoefu unaonyesha kuwa mapambano dhidi ya tawala za kiimla hufanikiwa tu pale harakati kama hiyo inaenda sambamba na kupambana dhidi ya utawala wa Kizayuni.
Hayo ni kwa mujibu wa Hujjatul Islam Mahdi Taeb, mhadhiri wa chuo kikuu, alipokuwa akizungumza mjini Tehran katika kikao cha ‘Kuchunguza Mwamko wa Ulimwengu wa Kiislamu’.
Akiashiria mwamko wa wananchi wa Bahrain, amesema mwamko huo unashika kasi siku baada ya siku na hivyo kutikisa misingi ya tawala za kiimla za Aal Khalifa na Aal Saud.
Amegusia ushindi wa taifa la Iran dhidi ya utawala wa kifalme na kiimla wa Pahlavi mwaka 1979 na kusema , ‘Aal Khalifa na Aal Saud hawana nguvu zaidi ya Wapahlavi’.
Amemtaja Imam Khomeini MA kuwa kiongozi mkubwa ambaye alitoa muongozo wenye busara uliopelekea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, mapinduzi ambayo sasa ni ilhamu kwa mwamko wa Kiislamu unaoshuhudiwa duniani.
Kikao cha ‘Kuchunguza Mwamko Katika Ulimwengu wa Kiislamu’ kimefanyika katika Chuo Kikuu cha Tehran.
788935
captcha