Kituo hicho kwa jila la Liqaa kimejengwa kwa udhamini wa Sultan Qaboos bin Said wa Oman na kwa uungaji mkono wa Rais Michel Suleiman.
Waliozungumza katika sherehe hizo wamesisitiza juu ya umuhimu wa kituo hicho na kusema kuwa kitawakurubisha pamoja Waislamu na Wakristo wa nchi hiyo. Pia wamesema kujengwa kwa kituo hicho nchini Lebanon kunadhihirisha msimamo mzuri wa rais wa nchi hiyo wa kushajiisha mazungumzo baina ya mirengo mbalimbali ya kidini na kiutamaduni katika kuondoa na kutatua tofauti zao.
Akizungumza katika sherehe hizo, Rais Michel Suleiman amesema kuwa kituo hicho kitatoa mchango mkubwa katika kuimarisha umoja wa kitaifa wa nchi hiyo na kwamba jambo hilo linaweza kuifanya nchi hiyo kuwa mfano bora wa kuigwa na mataifa mengine.
Viongozi na maafisa mbalimbali wa kidini, kiserikali, kisiasa na kijamii walishiriki katika sherehe za ufunguzi wa kituo hicho muhimu. 789832