IQNA

Wasomaji 36 wanachuana mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Saudia

12:44 - May 12, 2011
Habari ID: 2120998
Mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi, kosoma, tajwidi na tafsiri ya Qur'ani yalianza Jumanne ya wiki hii nchini Saudi Arabia yakiwashirikisha wasomaji 36.
Mashindano hayo yanayowashirikisha wasomaji wa kike na wa kiume yanasimamiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu katika sehemu tano mjini Riyadh.
Sehemu ya wanaume inashirikisha wasomaji 20 na ile ya wanawake ina wasomaji 16.
Mkuu wa Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Kuhifadhisha Qur'ani ya mkoa wa Jeddah Abdul Aziz Hanafi amesisitiza katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo juu ya umuhimu wa mashindano ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa. Amesema mashindano ya kitaifa ya Qur'ani ya Saudi Arabia yalianzia katika kiwango cha mikoa na kuingia awamu ya mwisho kitaifa.
Mashindano hayo ambayo yalianza kufanyika mwaka 1997 yanawashirikisha wanawake na wanaume kutoka maeneo mbalimbali ya Saudia. 790271

captcha