IQNA

Dini ya Kiislamu kuarifishwa kupitia televisheni ya Argentina

12:13 - May 14, 2011
Habari ID: 2121567
Kanali ya 7 ya televisheni ya Argentina imeanza kurusha hewani vipindi vilivyo na lengo la kuarifishwa Uislamu nchini humo.
Kwa mujibu wa tovuti ya ajib, vipindi hivyo vitakuwa vikitangazwa mara moja kila wiki kwa muda wa saa moja na Kituo cha Kiislamu cha Argentina ndicho kitakachokuwa na jukumu la kutayarisha na kuvidhamini.
Lengo la vipindi hivyo ni kuwafahamisha watu wasiokuwa Waislamu mafundisho ya dini ya Kiislamu zikiwemo nguzo za Uislamu, Qur'ani Tukufu, historia ya Uislamu na jamii ya Waislamu nchini Argentina.
Hii ni mara ya kwanza kwa vipindi kama hivyo kurushwa hewani kupitia televisheni ya taifa. Kituo cha Kiislamu cha Argentina kimewaalika wanazuoni, wasomi na wahubiri wa Kiislamu kushiriki kwenye vipindi hivyo ili kuuarifisha Uislamu nchini humo kwa njia iliyo bora zaidi.
Mapema mwezi huu Argentina ilipitisha sheria ya kuwaruhusu wanawake wa Kiislamu wanaovaa hijabu kuhudhuria shuleni na pia katika maeneo ya umma bila kukabiliwa na vikwazo vyovyote.
Kukubali serikali ya Argentina kurushwa vipindi vya Kiislamu katika televisheni ya taifa kunachukuliwa kuwa ni sehemu ya mipango ya serikali hiyo ya kuimarisha mazungumzo kati ya dini tofauti nchini humo. 790812
captcha