Kituo cha el Hikma kimeripoti kuwa kikao hicho kimesimamiwa na kituo cha Kiislamu cha el Hikma kikijadili maudhui ya sharia za Kiislamu kuhusu ndoa. Washiriki katika kikao hicho wamewasilisha pia maswali yao kuhusu maudhui hiyo.
Sehemu nyingine ya kikao hicho ilihusu warsha ya umuhimu wa familia katika Uislamu na vazi la hijabu la mwanamke wa Kiislamu katika nchi za Magharibi na za Kiislamu.
Jumuiya ya al Hikma ni miongoni mwa jumuiya muhimu za Kiislamu za Ubelgiji ambayo hujihusisha na kazi za mafunzo ya Qur’ani, lugha ya Kiarabu, kuitisha vikao vya kidini hususan kwa ajili ya wanawake na wanaume wa Kiislamu na kadhalika. 791243