Watayarishaji wa mnada huo wanasema kuwa mapato yake yatatumwa kwa wananchi wa Bahrain hususan wanaunzi wa vyuo vikuu waliopatwa na masaibu kutokana na matukio ya hivi karibuni nchini humo.
Wamewataka watu wote kushiriki katika mnada huo kwa kuweka bidhaa zao au kutoa msaada wa fedha kwa ajili ya wananchi wa Bahrain.
Hapo kabla pia wasanii wa Kisaudi Arabia walipiga mnada bidhaa zao katika mtandao wa Facebook na kutoa mapato yake kwa watu waliopatwa na maafa ya mafuriko wa Jeddah. 791209