IQNA

Awamu ya mwisho ya mashindano ya kiraa ya tartili kuanza Imarati

13:31 - May 15, 2011
Habari ID: 2122425
Awamu ya mwisho ya mashindano ya kiraa ya kuvutia zaidi ya tartili ya Qur'ani Tukufu inaanza leo ikisimamiwa na Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani, Tuzo ya Dubai.
Mwenyekiti wa kamati inayosimamia mashindano hayo Ibrahim Muhammad Bumalha amesema, mashindano hayo yataanza leo baada ya swala ya Magharibi katika msikiti wa Hassan al Sheikh katika mji wa Dubai.
Amesema kuwa kamati inaosimamia mashindano hayo imeweka televisheni kubwa katika msikiti wa Hassan al Sheikh ili kuwawezesha wanawake pia kufuatilia mashindano hayo.
Ahmad Saqar al Suwaidi ambaye ni miongoni mwa wanachama wa kamati inayosimamia mashindano hayo amesema wasomaji 552 walishiriki katika awamu ya kwanza ya mshindano haya na kwamba awamu ya mwsho inawashirikisha vijana na maimamu wa misikiti.
791791
captcha