IQNA

Chuo Kikuu cha Kiislamu Tanzania chasajili wanafunzi

13:55 - May 15, 2011
Habari ID: 2122462
Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro nchini Tanzania kinasajili wanachuo wapya kwa ajili ya mwaka wa masomo wa 2011/2012.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika tovuti ya chuo hicho, wanafunzi ambao ni raia wa Tanzania na wa kimataifa wanaweza kutuma maombi yao kwa ajili ya taaluma mbalimbali za shahada ya kwanza. Kati ya taaluma zinazofunzwa katika chuo hicho kiwango cha Shahada ya Kwanza ni Mawasiliano ya Habari, Sheria za Kiislamu, Dini ya Kiislamu, Masomo ya Biashara, Lugha na Ukalimani, Sanaa na Elimu za Jamii, Sayansi na Elimu.
Wanaotaka kujisajili wanapaswa kuwa na cheti cha shule ya upili ambacho kitaidhinishwa na Baraza la Senate la Chuo Kikuu.
Siku ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 31 Mei 2011. Fomu za wanaotaja kujisajili zinapatikana katika tovuti ya http://www.mum.ac.tz

Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro Tanzania kilianzishwa Oktoba 2004 na Waqfu wa Maendeleo ya Waislamu MDF. Lengo la kuanzishwa chuo hicho limetajwa kuwa ni kuhimiza elimu na ubunifu katika jamii ya Waislamu Tanzania na kieneo. Aidha chuo hicho kinalenga kuwatayarisha wasomi ambao watazingatia maadili ya Kiislamu katika maisha yao.
792020

captcha