IQNA

Kongamano la "Uislamu na Magharibi: Mazungumzo ya Kistaarabu"

14:48 - May 16, 2011
Habari ID: 2123203
Mji mkuu wa Imarati, Abu Dhabi utakuwa mwenyeji wa kongamano lenye anwani ya "Uislamu na Magharibi: Mazungumzo ya Kistaarabu".
Kongamano hilo ambalo limeanza leo Mei 16 limeandaliwa na Taasisi ya Utafiti na Masomo ya Kistratijia Imarati (ECSSR) kwa ushirikiano na Kitivo cha Sera na Masuala ya Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Maine cha Marekani.
Wataalamu wa masuala ya Kiislamu, uhusiano wa kimataifa na mazungumzo ya kistaarabu kutoka vyuo vikuu vya eneo la Ghuba ya Uajemi, Mashariki ya Kati, Ulaya na Marekani wanadhuhuria kongamano hilo la siku mbili.
Kati ya mada zitakazojadiliwa ni pamoja na "Nafasi ya Historia na Idiolojia katika Ukuruba wa Staarabu", Nafai ya Uchumi na Utamaduni, Ustawi wa Jamii katika Kuimarisha Mazungumzo ya Staarabu", 'Suala la Uraia kwa Mtazamo wa Uislamu na Magharibi na 'Upotoshaji katika Vyombo vya Habari".
792135
captcha