IQNA

Maqari wa Qur'ani waenziwa Deoband, India

19:10 - May 17, 2011
Habari ID: 2123816
Maqari bingwa wa Madrasa ya Dar-es-Salam katika mji wa Deoband nchini India walienziwa katika sherehe iliyofanyika jana Mei 16.
Kwa mujibu mwandishi wa IQNA, tawi la kusini mwa Asia, hafla hiyo imefanyika katika madrasa hiyo baada ya sala za Magharibi na Isha.
Kikao hicho kilianza kwa qiraa ya Qur'ani Tukufu ya Maulana Jamaluddin na kufuatiwa na hotuba ya Maulana Aslam Qasim mkuu wa Chuo cha Darul Ulum cha mji wa Deoband.
Maulana Qasim amesema kuwa siri ya mafanikio ya mwanadamu ni kujifunza na kutekeleza mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Amesema kutekeleza mafundisho ya Qur'ani kutawaletea Waislamu ustawi katika maisha yao.
793183
captcha