IQNA

Banki ya Kiislamu ya Sudan kufungua tawi Kenya

14:33 - May 18, 2011
Habari ID: 2124594
Banki ya Kiislamu ya Sudan yenye makao yake mjini Khartoum imetangaza kuwa inapanga kufungua tawi Kenya katika hatua ambayo itakuwa ya kwanza katika soko la sekta ya fedha ya Kiislamu Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa tovuti ya Islamic Globe, Kenya iko katika mkakati wa kubadilisha sheria zake za kifedha ili kuruhusu mfumo kamili wa kifedha wa Kiislamu kufanya kazi nchini humo.
Tayari Kenya ina benki miali za Kiislamu na vilevile shirika la bima la Kiislamu. 'Tunapanga kuingia Kenya ambapo tutatoa huduma za misaada ya kifedha katika biashara na vilevile huduma za uwekezaji ', amesema Fadi Sali al-Faqih Mkurugenzi Mkuu wa Banki ya Kiislamu ya Sudan.
Banki ya Kiislamu ya Sudan ilibinafsishwa mwaka 2002 na asilimia ya hisa zake zinamilikiwa na Banki ya Kiislamu ya Dubai. Hatua ya kuingia Kenya inahesabiwa kuwa ni katika mpango wa Benki ya Kiislamu ya Dubai kutumia fursa ambazo zinajitokeza katika huduma za kifedha za Kiislamu barani Afrika.
Wataalamu wanasema Waislamu barani Afrika sasa wanataka huduma za kifedha za Kiislamu kutokana na mwamko wa Kiislamu katika bara hilo.
794297
captcha