IQNA

Waziri wa Afya wa Iran:

Qur’an ndio njia bora zaidi ya kufikia umoja

15:09 - May 18, 2011
Habari ID: 2124626
Waziri wa Afya wa Iran amesema kuwa Waislamu wanapaswa kukusanyika chini ya kivuli cha Qur’ani ili waweze kufikia umoja na mshikamano.
Daktari Bi Marzia Dastejerdi ameyasema hayo katika ujumbe wake kwa Tamasha ya 16 ya Vyuo Vikuu vya Sayansi ya Tiba nchini Iran. Amesema katika kipindi hiki ambacho Waislamu wanahitaji umoja ili kukabiliana na maadui, njia bora zaidi ya kufikia umoja huo ni kupitia Qur’ani Tukufu na kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu kama ambavyo tunasoma katika Qur’ani Tukufu kuwa, “Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu na wala msitenganike”. Al Imran 103.
Ametoa wito kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kujifunza Qur’ani wakiwa bado vijana kwani wakati huo nyoyo zao huwa katika machipuo ya umaanawi.
Ameelezea matumaini yake kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watatekeleza mafundisho ya Qur’ani katika maisha yao. Amesema Qur’ani Tukufu ni kitabu cha kuponya, kuongoza na kuokoa wanadamu.
Tamasha ya 16 ya Vyuo Vikuu vya Sayansi ya Tiba nchini Iran imeanza leo Mei 18 katika mji wa Kashan.
793839
captcha