Licha ya maonyo ambayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na taasisi za Kiislamu za Ufaransa kwa serikali ya Paris ili ichukue hatua ya kulinda misikiti na maeneo ya ibada ya Waislamu lakini serikali hiyo imekataa kuchukua hatua yoyote kuhusiana na suala hilo na hivyo kupelekea misikiti ya Waislamu kushambuliwa katika miji tofauti ya nchi hiyo.
Kwa kutumia fursa ya kimya hicho cha serikali, baadhi ya watu wenye chuki na uadui dhidi ya Waislamu na Uislamu hivi karibu walishambulia msikiti uliotajwa na kuandika kwenye kuta zake maandishi ya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu yakiwemo yale yaliyosema, 'Ufaransa ni ya Wafaransa tu' na 'Mauti kwa Waislamu na Waarabu.'
Mara baada ya kuandikwa maandishi hayo Jumuiya ya Kiislamu ya al-Hijra na ofisi ya meya wa mji huyo walipeleka mashtaka yao mahakamani wakitaka wahalifu wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua ifaayo.
Tukio hilo la maandishi ya chuki na michoro ya misalaba iliyovunjika lililotokea usiku wa kuamkia Jumanne lilionekana kwa mara ya kwanza na waumini waliofika msikitini hapo kwa ajili ya kuswali swala ya asubuhi. 794220