IQNA

Umuhimu wa kufahamu ujumbe wa Qur'ani

12:38 - May 21, 2011
Habari ID: 2124953
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu cha Islamabad Pakistan Prof. Fateh Muhammad Malik amesisitiza umuhimu wa kufahamu ujumbe halisi wa Qur'ani Tukufu chini ya muongozo wa Mtume Mtukufu SAW.
Akizungumza katika hafla ya kutoa vyeti katika Taasisi ya Da'awah ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu cha Islamabad, amewapongeza waliofuzu na kusema: 'tunapaswa kufuata mafundisho ya Uislamu ili kukabailiana na changamoto zilizopo katika umma wa Waislamu".
Prof. Malik ameendelea kusema kuwa: 'tunapaswa kujiepusha na taasisi ambazo zinawapotosha Waislamu kupitia tafsiri mbovu ya ujumbe wa Qur'ani Tukufu.
Akizungumza katika kikao hicho Prof. Shahibzada Sajjid-ur-Rahman, mkurugenzi mkuu wa Chuo cha Da'awah cha Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu cha Islamabad amesema hii ni mara ya kwanza wanafunzi wa chuo hicho wanaosoma kwa njia ya posta kupata vyeti vya kuhitimu masomo.
794437
captcha