Mashindano hayo ambayo huzishirikisha shule za kidini, taasisi za hifdhi ya Qur'ani na wahubiri wa Kiislamu kote nchini Misri huandaliwa na Chuo Kikuu cha Kidini cha al-Azhar. Gazeti la al-Akhbar la Misri limesema kuwa Ahmad At-Tayyib, Sheikh wa al-Azhar ameafiki kuongezwa kwa bajeti hiyo hadi kufikia juneih milioni 21 za Misri.
Haddad Abdul Aal mmoja wa viongozi wa al-Azhar amesema kuwa kuna vitengo vingine vipya vitakavyoongezwa kwenye mashindano hayo kikiwemo cha tajwidi. Amesema tayari washindani wavulana na wasichana 190,000 kutoka madrasa na taasisi za hifdhi ya Qur'ani wamejiandikisha kushiriki katika mashindano ya mwaka huu. Amesema hatua ya mwanzo ya mashindano hayo ilifanyika katika chuo kikuu hicho ambapo washindi 13, 205walichaguliwa kushiriki katika hatua ya pili ya mashindano, ambapo wanazuoni na mashekhe wa al-Azhar wapatao 93 wamechaguliwa kuyasimamia.
Abdul Aal amesema mashindano hayo yatafanyika katika hatua tatu za kuhifadhi Qur'ani nzima, hifdhi ya juzuu 25 na hifdhi ya juzuu 18 ambapo washindi wanatazamiwa kupewa zawadi nono za pesa taslimu. 795062