Kongamano la uwekezaji katika nchi za Kiislamu limefanyika katika mji mkuu wa Jordan, Amman kwa lengo la kujadili mbinu mpya za kiuchumi, biasahra na uwekezaji.
Kongamano hilo limeandaliwa na Chumba cha Kiislamu cha Biashara na Viwanda cha Jordan na Chumba cha Biashara na Viwanda cha Kuwait.
Walid Al-Dabbous na Mahmoud Hamza wa Chumba cha Biashara na Viwanda Kuwait waliwakilisha serikali ya Kuwait katika kikao hicho.
Al Dabbous amesisitiza kuhusu kupanuliwa upeo wa ushirikiano wa kiuchumi, biashara na uwekezaji katika nchi za Kiislamu.
Amesisitiza kuhusu umuhimu wa kuarifishwa fursa za kibiashara baina ya taasisi za kifedha za Waislamu.
796010