Washiriki wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani pia watashiriki katika hafla hiyo itakayofanyika Jumanne 23 Mei.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Tabligh na Muongozo wa Kiislamu katika Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu Mohammad al Mahmoud amesema lengo la hafla hiyo itakayofanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Utamaduni cha Qatar ni kuwahimiza vijana kusoma na kujifunza Qur'ani Tukufu.
Mohammad Yahya Mohammad Taher aliyechukua nafasi ya kwanza kuhifadhi kikamilifu Qur'ani Tukufu katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Kuwait na Mohammad Abdul Rashid Sufi aliyechukua nafasi ya tatu wataenziwa.
796072