IQNA

Duru ya 19 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Chuo Kikuu cha al-Azhar

18:40 - May 23, 2011
Habari ID: 2127285
Mashindano ya kimataifa ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu ya Chuo Kikuu cha al-Azhar yamepangwa kufanyika tarehe 19 hadi 25 Agosti huko London mji mkuu wa Uingereza.
Mashindano hayo yatakayofanyika katika vitengo vitano kwa washiriki walio na umri wa chini ya miaka 25 yatachukua muda wa siku 6.
Washiriki wa mashindano hayo watachuana katika hifhi ya Qur'ani nzima huku wakichunga sheria za tajwidi na tartili na kufasiri juzuu ya 15 ya kitabu hicho kitakatifu, hifdhi ya Qur'ani nzima wakichunga sheria na kanuni za tajwidi na tartili, hifdhi ya juzuu 20 za mwanzo kwa kuchunga kanuni za tajwidi na tartili, hifdhi ya juzuu 10 za mwanzo wa Qur'ani kwa kuchunga sheria za tajwidi na tartili na hifdhi ya juzuu 6 zinazofuatana za Qur'ani kwa kuchunga sheria za tajwidi na tartili.
Marefa mashuhuri wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani watasimamia mashindano hayo na washindi watatangazwa mwishoni mwa mashindano.
Masharti ya washiriki wa mashindano hayo ni kuwa wasiwe ni wasomaji mashuhuri wa kimataifa, wahadhiri wa somo la tajwidi na tartili, washiriki katika duru zilizopita za masomo hayo wala wahitimu wa Chuo Kikuu cha al-Azhar. 796771
captcha