Idara hiyo itaanzishwa kwa amri ya Mfalme Hamad bin Isah Aal Khalifa wa nchi hiyo. Amri hiyo inatolewa katika hali ambayo askari jeshi wa nchi hiyo wakishirikiana na wa Saudi Arabia wamekuwa wakichoma moto Qur'ani Tukufu na kubomoa misikiti ya nchi hiyo. Utawala wa nchi hiyo haujachukua hatua yoyote ya kukabiliana na wahalifu.
Kwa kuzingatia mazingira ya hivi sasa ya Bahrain ambapo wapinzani wanakandamizwa na matukufu ya Kiislamu kuvunjiwa heshima kwa amri ya mfalme huyo, amri yake ya hivi sasa ya kuanzishwa idara ya Qur'ani katika wizara iliyotajwa inatambuliwa na wataalamu wa mambo kuwa ni hatua ya ujanja kwa madhumuni ya kuhadaa fikra za waliowengi na kufunika jinai za utawala huo za kuchoma moto Qur'ani na kubomoa misikiti ya Waislamu wa madhehebu ya Shia. 796772