Katika kuendeleza uingiliaji wake katika mambo ya ndani ya Bahrain, utawala wa kifalme wa Saudi Arabia umetoa pendekezo la kubadilishwa muundo na rangi za bendera ya nchi hiyo ili kufuta utambulisho wa mapinduzi ya wananchi wa nchi hiyo.
Watawala wa Saudia wamekuwa wakiingiwa na wasiwasi mkubwa kwa kuona rangi za bendera hiyo zikipeperushwa na wanamapinduzi wa Bahrain pamoja na waungaji mkono wao katika pembe mbalimbali za ulimwengu. Saudi pia inataka kuona kuwa wabunge wa Kishia ambao ndio wengi nchini Bahrain wakizuiwa kushiriki kwenye vikao vya bunge.
Pendekezo hilo la Saudi Arabia linabainisha wazi udhaifu mkubwa alionao Mfalme Hamad bin Isa Aal Khalifa wa Bahrain katika uendeshaji nchi na jinsi nchi hiyo inavyotegemea kwa kiwango kikubwa Wasaudia katika uendeshaji wa masuala yake ya utawala.
Kwa kutilia maanani kwamba serikali ya Bahrain hivi karibuni ilibomoa mnara wa Lulu katika Medani ya Lulu iliyochukuliwa kuwa nembo ya mapinduzi ili kuondoa uwezekano wa wanamapinduzi kukusanyika katika eneo hilo, kuna uwezekano mkubwa wa watawala wa nchi hiyo pia kukubali pendekezo la hivi karibuni la Saudia la kubadilishwa rangi za bendera yao ya kitaifa. 796940