IQNA

Mashindano ya Qur'ani kufanyika Marekani mwezi wa Ramadhani

14:16 - May 24, 2011
Habari ID: 2127565
Waislamu wa Marekani wamepanga kuandaa mashindano ya Qur'ani tarehe 14 Agosti inayosadifiana na tarehe 14 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mashindano hayo ya hifdhi ya Qur'ani yatafanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Naperville ICN katika jimbo la Illinois. Lengo la kufanyika mashindano hayo ni kuwashajiisha Waislamu wasome na kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa misingi ya sheria na kanuni za usomaji wa kitabu hicho kitakatifu. Walimu mashuhuri wa hifdhi na usomaji Qura'ni ndio wataokasimamia uamuzi wa mashindano hayo. Washindi wa mashindano hayo ambayo yanatazamiwa kufanyika katika makundi manne ya hifdhi ya juzuu tofauti za Qur'ani watapewa zawadi mwishoni mwa mashindano hayo.
Kituo hicho cha Kiislamu pia kimepanga kuandaa masomo ya mafunzo ya usomaji na hifdhi ya Qur'ani tokea tarehe 13 Juni hadi tarehe 4 Agosti. 796959
captcha