Mahakama hiyo imetangaza kuwa kuna udharura wa kufuatiliwa kesi hiyo ambapo mbunge huyo amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuchochea vitendo vya ubaguzi dhidi ya Waislamu na kuukosea heshima Uislamu.
Jean Morris jaji anayeendesha kesi hiyo amekanusha madai ya Bram Moszkovicz wakili wa Wilders kwamba mahakama hiyo haiendeshi kesi hiyo kwa uadilifu.
Kesi hiyo ilianza mwezi Oktoba mwaka uliopita baada ya Waislamu na watu wenye misimamo ya wastani nchini Uholanzi kufikisha mahakamani mashtaka yao dhidi ya mbunge huyo aliye na uadui mkubwa na Uislamu. Miongoni mwa mashtaka yaliyowasilishwa mahakamani dhidi ya Wilders ni pamoja na ubaguzi wake dhidi ya Uislamu na Waislamu, kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu na utengenezaji wa filamu ya Fitna inayovunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
Hivi karibuni mbunge huyo pia alitoa matamshi ya dharau na ubaguzi dhidi ya Waislamu alipokuwa akitoa mchango wake bungeni kuhusiana na suala la muundo wa Waislamu katika jamii ya Uholanzi. 797601