Larijani amesisitiza kuwa sera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuendelea kushirikiana na IAEA. Hata hivyo ameongeza kuwa taifa la Iran litaendelea kulinda mafanikio yake.
Ripoti yenye kurasa sita ya IAEA inadai kuwa wakala huo umepokea habari kuwa huenda mradi wa nyuklia wa Iran vilevile unafuata malengo yasiyo ya kiraia.Ripoti hiyo ilirudia kile inachosema ni tathmini jumla na kudai kuwa IAEA haiwezi kuthibitisha shughuli zote za nyuklia za Iran ni za malengo ya amani.
Itakumbukwa kuwa Marekani na waitifaki wake, ukiwemo utawala wa Kizayuni wa Israel, wamekuwa wakieneza madai yasiyo na msingi kuwa eti Iran ina malengo ya kijeshi katika shughuli zake za nyuklia. Hii ni katika hali ambayo IAEA imetuma wakaguzi wake katika vituo vya nyuklia vya Iran na hawajawahi kupata chochote kinachoashiria kukengeuka mkondo miradi ya nyuklia ya Iran.
798503