Nakala za Qur’ani zinazonasibishwa kwa Maimamu watoharifu (as) zinazohifadhiwa katika Haram ya Imam Ridha (as) katika mji mtakatifu wa Mash’had pia zitaonyeshwa katika maonyesho hayo.
Katika maonyesho hayo ambayo yanasimamiwa na Haram ya Imam Ridha (as) na Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ya Iran, kutakuwepo kazi 40 za michoro ya sana iliyotumika katika Qur’ani Tukufu, nakala za Qur’ani za kuanzia karne ya tatu Hijria hadi hii leo, nakala za Qur’ani zinayonasibishwa kwa Imam Ali bin Abi Twalib (as), Imam Hassan (as), Imam Ridha (as), Imam Mussa bin Ja’far (as) na Imam Sajjad (as).
Mtaalamu wa sanaa za Qur’ani kutoka Iran pia atakuwepo katika maonyesho hayo kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu sanaa hiyo. 798053