IQNA

Siri za maumbile katika Qur'ani zachunguzwa Imarati

12:51 - May 26, 2011
Habari ID: 2128789
Kikao cha kuchunguza siri za maumbile katika Qur'ani Tukufu kilianza Jumanne ya wiki hii katika kongamano la Miujiza ya Kisayansi ya Qur'ani huko Sharja, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Wataalamu na wasomi mbalimbali akiwemo Muhammad Khalid na Hamiid al Nuaimi walitoa hotuba mwanzoni kwa kongamano hilo wakijadili siri za mambile katika Qur'ani Tukufu.
Al Nuaimi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Akademia ya Chuo Kikuu cha Sharja amesema, baada ya kukamilisha masomo ya juu mwanadamu hutambua kwamba ndio kwanza yuko mwanzoni mwa kutafuta elimu na kwmaba anahitajia ufahamu tofauti. Amesisitiza kuwa tunapotazama maumbile ya dunia hii kama mbingu, nyota na sayari zake ndipo tunapotambua uhusiano wa karibu mno wa aya za Qur'ani na maumbile hayo na hatimaye kuona kudra na uwezo mkubwa wa Mwenyezi Mungu Muumba.
Khalid al Ubaid ambaye ni msomi na mhakiki wa masuala ya Qur'ani wa Imarati pia amehutubia kongamano hilo akizungumzia mfumo wa uhandisi katika Qur'ani Tukufu.
Kongamano la Miujiza ya Kisayansi ya Qur'ani limesimamiwa na Ofisi ya Masuala ya Utamaduni ya Baraza Kuu la Masuala ya Familia la Sharja likisaidiwa na Benki ya Kiislamu na Taasisi ya Marami ya mji huo. 798220
captcha