Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mkutano huo wa kimataifa utafanyika katika Chuo Kikuu cha Nairobi kuanzia Juni4-5. Lengo la mkutano huo limetajwa kuwa ni pamoja na kueneza ufahamu sahihi wa sayansi za Qur’ani katika vyuo vikuu nchini Kenya. Makala zaidi 30 zimewasilishwa katika sekretarieti ya kongamano hilo ambapo 10 ni kutoka Kenya, 8 kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na 7 kutoka nchi kama Nigeria, Tanzania bara na visiwani, Afrika Kusini na Oman.
Kongamano hilo litafunguliwa kwa hotuba ya Naibu Kansela ya Chuo Kikuu cha Nairobi Profesa Magoha na Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya Mheshimiwa Mohammad Khoshamadi. Wanazuoni waandamizi wa Kiislamu nchini Kenya watakaowasilisha makala katika kongamano hilo ni pamoja na Dr. Abdulkadir Hashim, Prof. Adam M. Adam, Prof. Mohammed S. Badamana na Dar. Sheikh Abdallah Kheir. A. Wasomi hao watawasilisha makala kuhusu mada mbalimbali za sayansi na Qur’ani Tukufu kwa kuzingatia changamoto za kisasa.
799054