IQNA

Viongozi wa kidini kukutana Ubelgiji

11:51 - May 28, 2011
Habari ID: 2129421
Viongozi wa dini za mbinguni na baadhi ya taasisi za kidini watakutana siku ya Jumatatu Mei 30 huko Brussels katika makao makuu ya Kamisheni ya Umoja wa Ulaya.
Kikao hicho ambacho kitafanyika baina ya viongozi wa Kiislamu, Kikristo, Kiyahudi na Kibudha na maafisa wa Umoja wa Ulaya kinalenga kuandaa uwanja wa kufanyika mazungumzo ya wazi kati ya viongozi wa kisiasa na viongozi wa kidini wa nchi wanachama wa umoja huo.
Zaidi ya viongozi wa kidini 20 wa nchi 13 wanachama wa Kamisheni ya Ulaya watashiriki katika kikao hicho kwa mujibu wa mada ya 17 ya Mkataba wa Lisbon ambayo inasisitiza juu ya kuandaliwa uwanja unaofaa kwa madhumuni ya kufanyika mazungumzo ya wazi kati ya viongozi wa Ulaya na taasisi za kidini za nchi wanachama. Washiriki watajadili matatizo na changamoto zinazowakumba wafuasi wa dini zilizotajwa barani Ulaya.
Wawakilishi wa Bunge, Baraza, na Kamisheni ya Ulaya watashiriki katika kikao hicho. 799300
captcha