Hafla hiyo imeandaliwa katika Chuo cha Qur’ani cha Dar-es-Salaam mjini Louga na kuhudhuriwa na wanafunzi, wanazuoni wa kidini pamoja na maafisa wa serikali.
Kati ya programu muhimu katika hafla hiyo ni qiraa ya Qur’ani Tukufu ya makari mashuhuri wa Senegal na vilevile qiraa ya wanafunzi wa Chuo cha Qur’ani cha Dar-es-Salaam. Aidha kumefanyika warsha yenye anwani ya ‘Mafunzo ya Qur’ani na Ustawishwaji Amani na Utulivu wa Kijamii’.
Pembizoni mwa kikao hicho, Waziri wa Afya wa Senegal vilevile amezindua kitengo cha tiba na afya katika chuo hicho.
Makumi ya maelfu ya watoto husoma qiraa na hifdhi ya Qur’ani katika vyuo vya Qur’ani nchini Senegal. Karibu asilimia 94 ya wakazi wa Senegal ni Waislamu.
799097