IQNA

Msahafu wa Masjidul Aqsa kuchapishwa Ghaza

19:41 - May 28, 2011
Habari ID: 2129752
Taasisi ya Uhakiki wa Kiislamu iliyochini ya Idara Kuu ya Uhakiki, Uandishi na Tarjumi ya al Azhar nchini Misri imepasishwa kuchapishwa msahafu wa Masjidul Aqsa katika eneo la Ukanda wa Gaza.
Gazeti la al Anbaa linalochapishwa nchini Kuwait limeripoti kuwa wakazi wa Ulanda wa Gaza wamefurahishwa mno na hatua hiyo ya Idara Kuu ya Uhakiki, Uandishi na Tarjumi ya al Azhar.
Nakala hiyo ya Qur'ani imeandikwa katika msikiti mtakatifu wa al Aqsa na itakuwa na picha ya msikiti huo katika jalada lake la mbele ya picha ya Qubbatul Swakhra katika jalada la nyuma.
Tayari imeanzishwa kamati maalumu ya kutathmini msahafu huo ambayo inaongozwa na Sheikhul Qurrai wa Misri Ahmad al Miisrawi.
Inatazamiwa kuwa msahafu huo wa Masjidul Aqsa utapokewa na wakazi wengi wa Palestina. 799735


captcha