Idara ya Uchunguzi ya al-Azhar imechukua uamuzi wa kubuni kamati hiyo kutokana na maombi na vilevile malalamiko ya raia wa Misri kuhusiana na kasoro nyingi walizonazo baadhi ya walimu wa mafunzo ya Qur'ani katika utekelezaji wa majukumu yao.
Baada ya kubuniwa kamati hiyo maafisa wake watakuwa wakitembelea vituo vyote vya mafunzo na hifdhi ya Qur'ani vinavyosimamiwa na al-Azhar na kuchunguza kazi za walimu wa mafundisho ya Qur'ani katika vituo hivyo.
Kamati hiyo itakayobuniwa hivi karibuni itatakiwa kutoa ripoti kuhusu tathmini yake ya vituo vilivyotajwa na kisha kuiwasilisha kwa viongozi husika kabla ya kuanza mwaka ujao wa masomo nchini Misri. 800058