IQNA

CD za mashindano ya usomaji bora wa Qur'ani zasambazwa Imarati

17:53 - May 29, 2011
Habari ID: 2130372
Albamu za CD za mashindano ya tartili bora ya Qur'ani zimesambazwa nchini Imarati na Taasisi ya Habari ya Jumuiya ya Kimataifa ya Qur'ani ya Zawadi ya Dubai.
CD hizo zinajumuisha visomo tofauti vya washiriki wa duru ya nne ya mashindano hayo ya tartili bora ya Qur'ani nchini Imarati. CD zilizosambazwa na taasisi iliyotajwa zina uwezo wa kutumika kwenye kompyuta na mitambo ya gari. Taasisi hiyo imetayarisha CD hizo kutokana na maombi ya washiriki na pia raia wengine wa Imarati ambao hufuatilia kwa karibu ratiba za taasisi hiyo. CD hizo pia zitasambazwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu serikalini, maktaba za umma na mashirika mengine yaliyo na hamu ya kunufaika na CD hizo.
Duru ya tano ya mashindano hayo ilifanyika hivi karibuni na wasimamizi wa taasisi iliyotajwa ya Zawadi ya Dubai wako mbioni kuandaa duru nyingine ya mashindano hayo ya usomaji bora wa Qur'ani kwa mbinu ya tartili. Kamati hiyo tayari imetuma mialiko katika nchi 160 za dunia kwa ajili ya kuwaarifisha wasomaji Qur'ani wao bora ili washiriki kwenye mashindano yajayo. 800099
captcha