IQNA

Wiki ya kulinda mapinduzi ya Bahrain yaanza

17:53 - May 29, 2011
Habari ID: 2130373
Wiki ya kulinda mapinduzi ya Bahrain ilianza jana Jumamosi chini ya usimamizi wa Muunano wa Vijana wa Mapinduzi ya 14 Februari.
Kituo cha habari cha al Aalam kimeripoti kuwa taarifa ya Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya 14 Februari pia imetangaza ratiba ya maandamano ya wananchi katika wiki ya kulinda mapinduzi ya Bahrain.
Taarifa hiyo imesisitiza juu ya kuakhirishwa maandamano makubwa ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika katika maeneo mbalimbali tarehe nchini Bahran.
Wakati huo huo wanaharakati wa masuala ya siasa wa Bahrain wameshiriki katika kikao kilichofanyika mjini Berlin Ujerumani na kuitaka nchi hiyo na Kamisheni ya Ulaya kuiwekea mashinikizo zaidi serikali ya Manama ili itimize matakwa ya wananchi wanaoendela kuandamana.
Washiriki katika kikao hicho pia wamesisitiza juu ya udharura wa kuchukuliwa hatua za kisiasa na za vyombo vya habari barani Ulaya haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kufichua jinai na uhalifu unaofanywa na utawala wa Aal Khalifa dhidi ya wananchi wa Bahrain. 800218

captcha